December 18, 2017

MBUNGE BULAYA WA CHADEMA ANAUMWA

Mbunge wa chadema Mh Esther Amosi Bulaya  leo tar 18/12/2017 yuko Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa operation ya Nyama za Pua,kwenye hospitali ya Taifa ya Africa Kusini!
Mh Bulaya Mbunge wa Jimbo la Bunda mjini kwa tiketi ya CHADEMA ,Alisafiri Jana kuelekea huko kwa ajili ya Matibabu!
Mh Bulaya mwanzo alifanyiwa upasuaji huo kwenye hospitali ya Taifa ya  Muhimbili Jijini Dar es salaam mnamo tar 08/10/2017 lakini hali bado haikutengemaa ndio maana ameenda kupata matibabu nchini huko ,!!
Mh Bulaya ameingia kwenye Chumba cha upasuaji  mchana huu kwa ajili ya kufanyiwa operation hiyo,Tuendelee kumuombea watanzania kwa ujumla wetu ,na wanabunda ili aweze kupona na kurejea kwenye majukumu yake ya kuwatumiakia wananchi wa Bunda na Tanzania kwa ujumla!!
Anategemea kurudi Tanzania baada ya majuma mawili!!

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE