December 9, 2017

MAGEREZA TUTAMUACHIA BABU SEYA LEO HIIMkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mboje amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumtoa gerezani Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha.
Mboje amesema hayo baada ya Rais John Magufuli kuwasamehe wafungwa hao ikiwa ni miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.
Akizungumza  leo Jumamosi jioni, Mboje amesema sasa hivi wanajaza fomu na itakapofika saa  11 watawaachia wafungwa hao.
Tayari ndugu jamaa na marafiki wa wanamuziki hao wako nje ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwasubiria.
Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE