December 18, 2017

LIPULI FC YASAJILI MAJEMBE 8

Image result for Lipuli FC Asante KwasiKLABU  ya  soko  la  Lipuli  Fc  ya  mkoani  Iringa imesema  tayari  imekamilisha  usajili  wa dirisha  dogo   kwa  kusajili  wachezaji nane  na  kuwaacha  wachezaji 6

Akizungumza na waandishi  wa  habari  jana  mjini  Iringa afisa  habari  wa  Lipuli  Fc  Clement  Sanga  alisema  kuwa  usajili  huo  umekamilishwa  toka  jumamosi  ya Desemba  16  kama  ambavyo  ratiba  iliyotolewa  awali na  TFF ilivyowataka  kukamilisha  usajili  huo.

 Sanga  alisema  kuwa  pamoja na  kuwepo  kwa maneno  mengi  kutoka kwa  wadau wa  soka na  wanachama  wa  Lipuli FC  kutaka  kujua  hatima ya  mchezaji raia  wa Ghana  Ahsante  Kwasi  ila  ukweli  bado  mchezaji  huyo ni mmoja  wa  wachezaji  wa Lipuli Fc  na  wakati  wowote  ataungana  na  wachezaji  wenzake  mjini  Iringa .

Aliwataja   wachezaji  waliosajiliwa  katika  dirisha  dogo  2017/2018  kuwa ni  Jamal Mnyate   ambae  amesajiliwa  kwa  mkopo  kutoka  Simba  SC , Adam Salamba  (mkopo  kutoka Stend United) Alex Ntiri (  Rai  wa  Ghana  kutoka  Mbao Fc )Miraji Mwilenga (kutoka  Mufindi  United), ZAwadi Mauya (kutoka  Mufindi  United), Steven Mganga (Pamba FC ), Nelson Mganga (mchezaji  Huru), Feisal Abdallah (Mchezaji  Huru kwa  sasa anachezea timu ya  Taifa  ya  Zanzibar )

Pia  aliwataja  wachezaji sita  waliotemwa  katika  kikosi  cha  Lipuli Fc  kuwa ni Waziri Ramadhan,Mussa Ngunda , Machaku Salum Machaku,Melvin Alistoto, Ahmed Manzi na Dotto Kayombo .

Katika  hatua  nyingine  Sanga  aliwaomba  wadau  wa  soka na  wapenzi  wa Lipuli  Fc  kuendelea  kutoa  ushirikiano  kwa  timu  hiyo  pamoja na  kuwaomba  wadhamini kuendelea  kujitokeza na  kudai  kuwa  lazima Lipuli  Fc  kuendelea kufanya  vema  katika msimu  ujao utakao anza  wakati  wowote  kuanzia .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE