December 25, 2017

kuwakumbuka wahamiaji

Pope Francis prays during a Christmas Eve Mass at St Peter's Basilica in the Vatican. Photo: 24 December 2017Papa Francis awataka wakatoliki kuwakumbuka wahamiaji                

Papa Francis amewahimiza waumini wa kanisa la Roma Katoliki wasiwatupia mgongo mamilioni ya wahamiaji ambao wamefukuza kutoka makaazi yao wakati wa misa kabla ya Krisma
Kiongozi huyo wa dini aliwafananisha wahamiaji na Maria na Yosefu kutoka Bibilia, na namna ambavyo walivyosafiri kutoka Nazareti hadi Bethlehemu bila kupata makazi.
 
Alieeleza kuwa wahamiaji wengi wanalazimika kukimbia viongozi wao ambao 'hawaoni tatizo na kumwaga damu ya wasio na hatia"
Papa Francis amefanya uteteaji wa wahamiaji kama maadhui yake kuu katika uongozi wake.
Nuns watch a procession at the Church of the Nativity in Bethlehem on December 24, 2017.Waumini wakiwa kwenye kanisa huko Bethlehem                
Idadi ya wakimbizi duniani imezidi milioni 22,ikiwa idadi kubwa ikitokea kwa warohingya kukimbia uhalifu nchini Myanmar.
"Nyayo zao zimefichwa kwenye nyayo za Yosefu na Maria,' alielezea Papa Francis, ambaye yeye pia ni mjukuu wa wahamiaji kutoka Italia, kwa washirika wa kanisa la St Peters mjini Vatican,jioni ya Jumapili.

Kiongozi huyo wa waumini waroma katoliki takriban bilioni 1.2 amesisitiza kuwa imani yao inataka wageni wakaribishwe kila mahali.
Papa Francis anatarajiwa kutoa hotuba yake ya "Urbi et Orbi" , yaani "kwa mji na kwa dunia" siku ya Jumatatu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE