December 31, 2017

KOREA KASKAZINI HAITAACHANA NA MPANGO WAKE WA KINYUKLIA

Image result for KOREA KASKAZINI
Korea Kaskazini imesema haitoachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ikiwa Marekani na washirika wake wataendelea kufanya mazoezi ya kijeshi karibu na nchi yake.
Shirika la habari la Korea Kaskazini limetoa taarifa hiyo leo wakati likifanya uchambuzi wa silaha kubwa za kinyuklia zinazomilikiwa na taifa hilo pamoja na majaribio ya makombora yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo kwa mwaka huu.

 Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake kubwa la makombora mnamo mwezi Septemba na kuzindua makombora matatu yenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine mwezi Julai na Novemba, yaliyozusha wasiwasi kwamba huenda nchi hiyo ikawa inamiliki bomu la kinyulia linloweza kurushwa hadi nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE