December 28, 2017

KESI YA MEYA IRINGA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA KUENDELEA JANUARY 11
KESI ya kutishia kumuua mtu kwa bastola inayomkabili Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe imeahirishwa kwa mara ya tatu hii leo hadi Januari 11, 2018.

Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa Novemba 28, kabla ya kuahirishwa hadi Desemba 12, mwaka huu.

Kimbe anashitakiwa kutenda kosa hilo Novemba 26 mwaka huu katika kata ya Kitwiru mjini Iringa wakati shughuli ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo ikiendelea.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 189 ya mwaka 2017 Kimbe anashitakiwa kutishia kumuua kwa bastola Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV CCM) Manispaa ya Iringa, Alphonce Muyinga kinyume na kifungu namba 89 (2) (a) cha kanuni za adhabu.

Akiomba kuahilishwa kwa kesi hiyo ya jinai namba 189 ya mwaka 2017  leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Richard Kasele, Wakili wa Serikali, Alice Thomas alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

“Mheshimiwa shauri hili bado lipo kwa ajili ya kutajwa, tunaomba liahirishwe kwa kuwa upelelezi wake bado haujakamilika,” alisema wakili huyo.

Tofauti na alivyofika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Meya huyo ambaye yupo nje kwa dhamana; jana alikuwa pekee yake wakati akiwasili mahakamani hapo kwa kutumia gari inayotumiwa na meya wa manispaa hiyo.


Ndani na nje ya viunga vya mahakama hiyo hapakuwepo na wafuasi wa chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati kesi hiyo ikitajwa kwa mara ya t

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE