December 17, 2017

Jacob Zuma asema mustakabali wa ANC upo katika tishio.

        Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja                                     Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja                

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio.
Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho.
Rais Zuma amezungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka.
Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura.
Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa.
Wagombea wakuu wanaopigiwa upatu kumrithi kama kiongozi wa chama hicho ni naibu rais, Cyril Ramaphosa, na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Nkosazana Dlamini-Zuma, mkewe Zuma wa zamani.
Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.
Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.
Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.
Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg.
Wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.
Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril RamaphosaWagombea wakuu ni Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril Ramaphosa                
Kivumbi hasa kipo katika Kinyanganyiro cha kumrithi rais Zuma, kama kiongozi wa chama- ni kati ya mkewe wa zamani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma -- ambae pia aliwahi kuwa waziri na vilevile alikuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika.

Lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa,
Mvutano huu pamoja na kashfa chungu nzima hasa za rushwa zinazomuandama rais Jacob Zuma zimeongoza hofu za kugawanyika kwa ANC.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE