December 27, 2017

HALI YAZIDI KUWA MBAYA SUDAN KUSINI, WAKIMBIZI WAMIMINIKA DRC

Image result for Kundi la wakimbizi kutoka Sudan Kusini baada ya kufika kwenye kambi moja nchini DRC kutorokea mapigano mjini Lasu. Wanaonekana hapa karibu na mji wa Aba, Dec. 23, 2017.

Tangu serikali ya Sudan Kusini kuikamata kambi ya waasi  Kusini Magharibi mwa nchi wiki iliyopita, mamia ya wakimbizi wameendelea kumiminika kwenye nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Miongoni mwao huenda wamo waasi, na jeshi la Kongo ambalo linahofia kusambaa kwa vita na kuingia nchini mwao, linakamata watu wote wanaoshukiwa kuwa wapiganaji.
Wakimbizi hata hivyo wanasema kuwa vijana wasiokuwa na hatia pia wamekamatwa wakati wa msako huo.
Ni vigumu kujua ni washukiwa wangapi waliokamatwa kufikia sasa.
Afisa mmoja wa serikali ya Kongo aliyezungumza kwa misingi ya kutotajwa jina kwa sababu haruhusiwi kuongea na wanahabari, alisema washukiwa tisa wako rumande ya kijeshi.
Viongozi kwenye kambi moja ya wakimbizi wamesema waasi 17 ndio waliokamatwa kufikia sasa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE