December 5, 2017

HAKUNA ANAYENUNUA WAPINZANI KAZI YA RAIS JPM INAUA UPINZANI -WAZIRI MAKAMBA

Waziri  Makamba  akifungua  mkutano wa CCM  mkoa  wa  Iringa
Mgombea  wa  NEC  mkoa  wa  Iringa  Salim Asas kulia  akiwa na  wagombea  wenzake
Mgombea  wa  NEC mkoa  wa  Iringa Marcelina  Mkini  akiomba  kura
Salim  Asas  akiomba  kura  leo
Wajumbe  wakipiga  kura
Wagombea  nafasi ya  kiti  mkoa
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Januari Makamba amesema  kazi nzuri  inayofanywa na  Rais Dkt  John Magufuli  ni  anguko  la  upinzani nchini .

Kwani  asema pamoja na upinzani  kulalamika kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ina nunua wapinzani ila hakuna mkakati wowote  wa  kununua mpinzani  ili kuua upinzani nchini mkakati  uliopo  ni  kuzidi  kuchapa kazi na  kuwatumikia watanzania kama ilivyosasa  kwa  Rais Dkt Magufuli .

Makamba  ambae pia  ni  mjumbe  wa  Halmashauri  kuu ya  Taifa ya  Chama  cha Mapinduzi ( NEC)  aliyasema  hayo  leo katika  ukumbi wa kichangani  mjini  Iringa wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi  wa CCM mkoa  wa  Iringa .
Alisema chini ya utawala wa Rais Dk John Magufuli, CCM inapata uhai mpya utakaokiwezesha kutawala katika kipindi cha miaka mingine 50.

“CCM inapata uhai mpya, kazi zinazofanywa na serikali ya Dk Magufuli ndizo zinazoua upinzani, watu wanauona na wana uelewa muelekeo wa Rais katika kujenga Taifa hili,” alisema.

Aliwataka wapinzani wasitafute visingizio na wasitoe malalamiko yasio na ushahidi wala msingi kwamba CCM inanua wapinzani.

“Hatufanyi hila, hatununui mtu, hakuna fitina wala figisufigisu, kazi tunazofanya zinazidi kuiimarisha CCM,” alisema


Alisema  kuwa hakuna  kiongozi  anayeua upinzani  nchini  isipo  kuwa  kazi  nzuri zinazofanywa na  Rais Dkt   Magufuli  ni kifo  kikubwa  kwa  upinzani hapa  nchini .

katika  mkutano  mkuu  wa  uchaguzi  wa CCM  mkoa  wa  Iringa alisema  kuwa CCM  mkoa  wa  Iringa  ilikuwa  ikihesabiwa  kama  ngome  ya  chama Taifa .

Hivyo  alisema  lazima  heshima  hiyo  kurejea  kwa  CCM kujipanga  kufanya  vyema  katika  chaguzi  mbali mbali  zijazo  .

Awali  akitangaza  kujiuzulu kamati ya  siasa  ya  mkoa kwa  niaba ya  wenzake  mkoa  wa  Iringa mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa akiaga kwa  niaba ya  wajumbe wa kamati ya  siasa ya  mkoa alisema  kuwa    utendaji kazi  wa serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  Magufuli ni  utendaji  ambao  una mvutia  kila  mmoja  na  hivyo  kutokana na kazi  kubwa  inayofanywa na serikali ya  CCM ndio sababu  inayopelekea  wapinzani  kuanza  kujiuzulu na hata  kujiunga na  CCM ili kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais .

 Masenza  alisema  kuwa kama  mkuu  wa  mkoa wa  Iringa yupo  bega  kwa  bega na  chama  pamoja na serikali   ili  kuona  CCM inaendelea  kushinda na  kuongeza  kuwa pamoja  ni  mwanamke  ila anapiga kazi  kama  mwanaume  na  kuona  hamuangushi Rais wala  chama .

“ Wanawake  tuna uwezo wa  kuongoza  na ndio maana  mkoa  wa  Iringa umeendelea  kufanya  vema katika mambo ya  kimaendeleo  na katika  siasa  na  tutazidi  kuonyesha  uwezo  wetu “

Katika mkutano  huo baadhi ya madiwani  wa  upinzani ambao  walikuwa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo  (Chadema)  Edga  Mgimwa  aliyekuwa  diwani kata ya  Kihesa  , Husna  Ngasi  aliyekuwa  diwani  wa  viti maalum Chadem na  Diwani  mteule wa kata ya  Kitwiru  Baraka  Kimata  walipata  nafasi  ya  kutambulishwa na kusalimia  wajumbe .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE