December 2, 2017

DONGO LA MAKAMU WA RAIS KWA WANAUME WATU WAZIMA


Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amewataka wanaume wa Tanzania kuacha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo, kwa kuona wakubwa wenzao hawana ladha ile wanayoitaka.
Mama Samia ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani,na kusema kwamba kitendo cha wanaume hao kuwafuata watoto wadogo licha ya kujua wameambukizwa ili tu kupata ladha yao, ni dhambi kubwa ambayo hata Mungu hawezi samehe.
"Wanaume na nyinyi muwe na maadili, wanaume wakubwa mnahisi labda wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwa hiyo mnahamia kwa wototo wadogo, huu si mwendo mzri, hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho, na wengine wanaijua kabisa kwamba wameshaambukizwa, na wakubwa wenzao wanajua wameambukizwa, wanashifti kwa watoto ambao hawawajui kwa kutumia vicent kidogo, huu ni uuaji wa makusudi na Mungu hatawasamehe katika hili waachieni watoto wetu wakue watunze taifa letu", amesema Mama Samia.
Hapo jana dunia imeadhimisha siku ya UKIMWI, ambapo sherehe hizo kitaifa zimefanyika jijini Dar es salaam katika viwanja vya mnazi mmoja, na Makamu wa Rais kuhudhuria kama mgeni rasmi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE