December 9, 2017

CUF WAWALILIA ASKARI WALIOUWAWA DRC

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)

THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

KUHUSU SHAMBULIZI NA MAUAJI YA WALINDA WA AMANI WA UN, WANAJESHI WA TANZANIA DR CONGO:

KATIBU MKUU MAALIM SEIFSHARIF HAMAD amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mashambulizi na mauaji ya Walinda Amani wa UN 14 na wengine 53 kujeruhiwa yaliyotokea katika Jimbo la Kivu, Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kufuatia shambulio hilo na maafa yaliyotokea Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa Rais DKT JOHN POMBE MAGUFULI, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa DKT Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali, Venance Salvatory Mabeyo, Maafisa na Askari wote wa JWTZ, familia na ndugu wa marehemu na Watanzania  wote kwa ujumla kwa kuwapoteza mashujaa waliokuwa wakitekeleza wajibu wao kwaniaba ya Taifa letu

“Tunaungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kulaani shambulio hilo ambalo ni sawa na uhalifu wa kivita na kuitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na wahusika wote kuchukuliwa hatua stahiki na kuwajibishwa...Natuma salamu zangu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waathirika wote na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kwa wale waliojeruhiwa nawatakia uponaji wa haraka ili warejee katika majukumu yao ya kawaida. Aidha, tunawaombea marehemu wote Mwenyenzi Mungu awapumzishe mahala pema peponi-Aamini” ameeleza Maalim Seif.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 8/12/2017
Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.

SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HABARI,
Zantel +255 777 414112 / Tigo +255 655 314112

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE