December 26, 2017

CHADEMA YAPATA PIGO , DIWANI SIHA AJIUZULU NA KUKIMBILIA CCM

Image result for kutoka chadema kwenda ccm
Mwenyekiti wa Wilaya ya Siha (CHADEMA), na Diwani wa Kata ya Gararagua ametangaza kujivua nafasi zake zote za uongozi ndani ya Chama hicho na kutangaza anahamia Chama Cha Mapinduzi kuungana na Rais Magufuli kulinda rasilimali za nchi.

Mwenyekiti Zakaria Lazaro Lukumay amesema kwamba anaamini kwamba CCM ndicho chama pekee ambacho kinagusa maisha ya watanzania hivyo ameamua kujiunga ili kutetea, kulinda, na kusimamia rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kupiga vita ufisadi, rushwa na mambo mengine yanayofanana na hayo.Katika taarifa yake aliyoituma kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha,  Lukumay ameongeza kuwa anaamini katika maamuzi yake aliyoyafanya atakuwa huru kuungana na Mh. Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE