December 24, 2017

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA DR PINDI CHANA ASEMA KENYA NI AMANI KWA SASA

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr Pindi Chana akitoa salam za watanzania waishio kenya Leo katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)  usharika wa kanisa kuu kulia ni ASKOFU mstaafu wa kanisa hilo Dr owdenburg Mdegella akimsikiliza 
Askofu Mstaafu KKKT Dayosisi ya Iringa Dr Mdegella akimpongeza balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr Pindi Chana Leo, ibadani 
Dr Chana akihojiwa na Mtandao wa matukiodaima Leo BALOZI  wa  Tanzania  nchini Kenya Dr  Pindi  Chana amewataka  watanzania kuendelea  kutumia  fursa  ya ushirikiano wa nchi  za  Afrika Mashariki kwa  kwenda  kufanya  biashara mbali mbali  nchini Kenya kwani hali ya amani na  utulivu nchini  humo  ni nzuri na ushirikiano wa nchi  ya Kenya na Tanzania umekuwa mkubwa  zaidi.

“ Awali  ya  yote  nimshukuru  Mungu  sana  kwa  kuniwezesha  kuja  nyumba   kwa  likizo ya Krismas  na mwaka  mpya  nitoe  salam nyingi kwa  wote heri ya  Krismas na mwaka mpya ila  pamoja na  salam hizi  nilete  salam za watanzania  wanaoishi Kenya  wanawasalim sana  tunao watanzania  wengi wa  kutosha  pale Jamhuri ya  Kenya na hawa  wanafanya kazi mbali mbali kwenye makampuni na taasisi  mbali mbali “

Akitoa  salam  hizo   leo baada ya karibishwa na askofu  mstaafu wa kanisa la  Kiinjili la   Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa Dk. Owdenburg Mdegella  kutoa  salam zake  kwa  waumini wa kanisa hilo usharika wa kanisa kuu  wakati  wa idaba  ya jumapili , Dr Chana  alisema  kuwa  baada ya  uchaguzi  kukamilika  nchini  Kenya hali ya amani na utulivu  imerejea na  wananchi  wanaendelea na shughuli  zao kama  kawaida  na  kuwa  kutokana na ushirikiano  uliopo Raia wa Kenya   wamekuwa  wakifanya shughuli  zao nchini Tanzania na  watanzania  wanafanya  shughuli  zao nchini  Kenya.

Hivyo si vibaya  kwa  wafanyabiashara  wa Tanzania  kutumia  fursa ya  kujitanua  kibiashara  kwa  kwenda  kufanyabiashara  zao Kenya kwa  kuungana na  watanzania  wenzao  waliopo  huko ambao  wanafanya biashara na  shughuli  nyingine kwa  uhuru kabisa .

  Watanzania  hawa  wanafanya kazi  mbali mbali biashara , ya  chai ,Kahama na  nyingine  na  kuwa  biashara  zao  zinaendelea  vema japo  wapo  wakenya  ambao  wanafanya shughuli  za uwekezaji  nchini Tanzania na sisi sasa  tunasema  ni Tanzania ya  viwanda  hivyo  tnawaalika  watu  waje  wawekeze katika  sekta ya viwanda hapa nchini ,tunayo mashirika yanayofanya kazi Tanzania   kupitia Diplomasia  ya  uchuni mfano  shirika la Ndege Kenya ambalo kwa sasa   linafaya safari  mara  sita  kwa  siku jambo ambalo la  kupongeza  sana pamoja na mashirika mengine”

Pia  alisema  kuna vitega  uchumi  vingi ambavyo  wakenya  wamewekeza  nchini kama Uchimi   Nakumati Supermarket pamoja na banki  nyingi ambazo zimewekezwa na  wakenya  hapa nchini jambo  ambalo  linaonyesha ni kwa kiasi gani nchi  hizi  zinaushirikiano mkubwa .

  Hawa  wawekezaji  wake  wametoka  Kenya  na  sasa  hivi  serikali yetu chini ya  Rais Dr John Magufuli inahamasisha  sana  watu kuja  kuwekeza nchini  kama  hatua ya  kuelekea Tanzania ya  viwanda na  ni  wawekezaji  wengi katika Tanzania ya uchumi  wanakuja  kuwekeza ukitaka  kutambua  hilo  kuwa  wakati wa uchaguzi sisi  Tanzania  wakati nchi zote  za jumuiya  ya Afrika mashariki  walikuwa na  kituo kimoja   cha kupigia kura  nchini Tanzania  kulikuwa na vituo  viwili kwa  ajili ya  wenzetu  wa Kenya  kituo kimoja kilikuwa Dar es Salaam na cha pili Arusha  hii ni uthibitisho  kuwa mahusiano yetu  yapo  imara  kisiasa , kijamii  na  kiuchumi “Akizungumzia  hali ya siasa nchini Tanzania  na Kenya  alisema  kuwa ukitanzama  uchaguzi uliofanyika Ujerumani , Zimbabwe , Afrika  kusini , Tanzania  ,Kenya na  nchini nyingine  utabaini  kuwa Demokrasia  nchini Tanzania  ni pana  zaidi  kwani  vyama  takribani 20 vimepata  kusajiliwa na  vyote  vinafanya siasa ya  bila  kubaguana na  ukitaka  kujua  kuwa  Demokrasia  Tanzania  imekuwa unaona  jinsi ambavyo  watanzania  wanavyoshirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii  ikiwemo misiba na  shughuli nyingine bila  kubaguana .

Kwa upande  wake askofu mstaafu Dk. Mdegella akihubiri  kanisani  hapo  alisema  kuwa   ni  vema  watanzania  kuendelea  kuombea  amani ya nchini  yetu  ili  amani  hii ambayo  ipo iendelee  kuwepo na  kuwa kazi  kubwa  imekuwa  ikifanywa na Rais Dr Magufuli katika kuona nchini inaendelea  kukuwa  kiuchumi pamoja na kuwa na amani zaidi.

Dr  Mdegella  alisema  kuwa  hivi  sasa  kumekuwepo na  ongezeko  la manabii  wa  uongo ambao  wanajipachika majina ya manabii  ambao kazi  yao  kubwa ni kudanganya  watu  kwa  kisingizio  cha  kupanda  mbegu jambo ambalo ni uongo mtupu kama kweli  wana  watu hao  ambao ni  viongozi wa dini  wanataka  kupanda  mbegu ni  vema  wakapanda  mbegu  zao kwa  kusaidia wasiojiweza  .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE