December 4, 2017

BAADA YA KUKABIDHIWA SIMBA ‘MO’ ATAJA MAMBO MAKUU 10 YAKUANZA NAYO

 
 DSC_0441-640x426
Bilionea Mohammed Dewji ameipokea kwa mikono miwili ishu yake ya ushindi kuwa mwekezaji mpya Simba na ametoa ahadi zake 10 kuhakikisha zinafanyika kuleta mabadiliko makubwa.

Mo Dewji ameshinda zabuni ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa dau la Sh bilioni 20 alizoweka ‘mezani’ na hakukuwa na mtu yoyote aliyejitokeza kushindana naye kama ilivyokuwa ikielezwa awali.MOJA:
Kambi ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi.
MBILI:
Simba sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.
TATU:
Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.
NNE:
Mo Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.
TANO:
Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.
SITA:
Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.

SABA:
Simba itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika.

NANE:
Ameahidi kutenga kitita cha  Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja kwa ajili ya usajili.

TISA:
Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.

KUMI:
Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE