November 14, 2017

ZIARA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI AIPONGEZA IDARA YA HABARI MAELEZO

Pix 01
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (kushoto) akipata maelekezo toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kulia) wakati alipoitembelea Ofisi za Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus Willium.
Pix 02
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema  leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 03
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus Willium.
Pix 04
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus Willium (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Susan Mlawi (katikati) alipotembea Ofisi za Idara hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
Pix 05
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) akisoma Jarida la Nchi Yetu wakati alipofanya ziara katika Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nicholaus Willium na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Pix 06
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 07
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholaus  Willium (kulia) nakala ya Jarida la Nchi Yetu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Susan Mlawi  katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa- MAELEZO
………………..
Katibu Mkuu Mlawi aipa Kongole Idara ya Habari Maelezo
Na.Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Bi. Suzan Mlawi, amepongeza utendaji kazi na ubunifu unaofanywa na Idara ya Habari- MAELEZO katika kuuhabarisha umma juu ya masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Tano.
Pongezi hizo amezitoa leo wakati alipokutana na uongozi wa Idara ya Habari- MAELEZO katika kikao kazi kilichokifanya  mahsusi kufahamu majukumu na changamoto zinazoikabili idara hiyo.
“Nyinyi ni idara muhimu sana na yenye majukumu makubwa sana ya kuisemea na kuitetea serikali hivyo mna jukumu la kufanya kazi kwa weledi, kwa kufuata Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma pamoja na taaluma na miiko ya uandishi wa habari ili muwe mfano kwa wanatasnia ya habari mnaowasimamia” alisema Bi. Mlawi.
Aliitaka Idara ya Habari kuhakikisha wanakuwa na vikao vya mara kwa mara na vyombo vya habari ili kushauriana namna nzuri ya kuendeleza tasnia ya habari lakini pia kukumbushana majukumu na wajibu wao kama wanahabari hasa katika kuzisukuma mbele ajenda mahsusi za serikali ya Awamu ya Tano, kama kujenga Tanzania ya viwanda, kudumisha uzalendo na mapenzi kwa nchi pamoja na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bi. Mlawi ambaye alifuatana na Naibu Katibu wake Bw. Nicolaus Wilium, alisisitiza umuhimu wa idara kuendeleza ubunifu katika mawasiliano yake na umma ili kuwawezesha wananchi wakiwemo wa vijijini kuwa na ufahamu mzuri wa mambo mengi makubwa na mazuri ambayo serikali imefanya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbassi  alisema ujio wa Katibu Mkuu kwenye idara yake ni faraja kwani unaongeza ari na motisha kwa wafanyakazi kujituma na  kufanya kazi kwa weledi zaidi.
“Nikuhakikishie ndugu Katibu Mkuu tumefarijika kwa ujio wako na tunaahidi kufanyia kazi yale yote uliyotuelekeza ili idara iweze kutekeleza majukumu yake yaliyowekwa kwa mujibu  wa sheria kwa maslahi mapana ya nchi “ alisema Dkt. Abbassi.
Katibu Mkuu na Naibu wake wako kwenye ziara ya kujitambulisha kwenye baadhi ya taasisi zilizoko chini yao, baada ya kuapishwa kushika nyadhifa zao mapema mwezi uliopita.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE