November 25, 2017

WANAO-BET WAKUTANA NA WAZIRI MWAKYEMBE


Wamiliki wa Kampuni za Michezo ya kubahatisha nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kusaidia ukuaji wa sekta ya Michezo.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na viongozi wa makampuni mbalimbali ya michezo ya kubahatisha nchini, ambapo wameongelea namna ya kukuza sekta ya michezo kwa maendeleo ya taifa kama inavyofanyika katika mataifa mengine.
‘’Najua nyinyi ni wadau wakubwa wa michezo japo mchezo huu wa kubahatisha ni mgeni katika taifa letu ila ni mchezo unaokua kwa kasi hivyo ningependa kuona mnatoa ushirikiano katika kukuza sekta ya michezo kwa taifa kwani sekta hii imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha na miundombinu,’’amesema Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri pia ametumia nafasi hiyo kuishukuru na kuipongeza Kampuni ya Mchezo wa kubahatisha ya Sportpesa kwa kutoa ufadhili wa kufanya matengenezo ya nyasi za uwanja wa Taifa zilizokuwa zimechakaa kufuatia maandalizi ya mashindano ya AFCON U17 ya 2019 yatakayofanyika nchini.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la ]waendesha Michezo ya Kubahatisha (TSBA) Bw.Dhiresh Kaba ameishukuru serikli kwa kusema, ‘’Naishukuru Serikali kwa kutupa nafasi ya kuweza kuchangia katika maendeleo ya michezo nchini sababu mchezo wetu unategema sana michezo na michezo ya nchini itakapopata

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE