November 19, 2017

WAANDAMANAJI WAPIGA KAMBI NJE YA MAKAZI YA RAIS MUGABE

                              

Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.
Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.
Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.
Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano.
Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.
Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi.
Waandamanaji wakiunga mkono jeshi
                    Waandamanaji wakiunga mkono jeshi
Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980.
Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni.
Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu -PF.
Waandamanaji wakimtaka rais Mugabe kujiuzulu wengi wakibeba mabango yakumtaka ang'atuke mamlakani                                     Waandamanaji wakimtaka rais Mugabe kujiuzulu wengi wakibeba mabango yakumtaka ang'atuke mamlakani                
Wapiganiaji wa uhuru ambao hadi kufiki mwaka uliopita walikuwa watiifu kwa rais Mugabe pia wanasema kwamba rais Mugabe anafaa kung'atuka mamlakani.

Kiongozi wa shirika hilo amewataka raia kuelekea katika makao ya rais Mugabe.
Nje ya ikulu ya rais kuna baadhi ya watu walioketi chini ili kuonyesha pingamizi yao mbele ya majeshi, huku kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai akihutubia umati mkubwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE