November 26, 2017

VIONGOZI SERIKALINI MUIGENI MAKONDA- JPM

nex
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, leo amemwagia sifa kedekede RC Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul MAKONDA.
Mh. JPM alizimwaga sifa hizo leo asubuhi alipokuwa akiwashukuru na kuwaaga madaktari wa meli ya China, ambao wametibu wagonjwa zaidi ya 5000 kwa wiki moja.
“Hata kama kuna watu hawampendi Mkuu wa mkoa wa PAUL  MAKONDA, lakini yeye anawapenda sana na anahangaika sana na wananchi wa mkoa wake”.
“Nilimuona wakati fulani akihangaika kuwatafutia miguu watu wake walemavu, nikajiuliza hivi huko kwingine hakuna walemavu?”.
“Nilipomuona wakati fulani alipoenda kiwanda cha magodoro Dodoma kuomba magodoro 1000 kwa ajili ya wagonjwa wa mkoa wake, nilijiuliza hivi kule Dodoma hawapo wagonjwa?”.
“Nilipomuona akienda kutengeneza magari ya polisi kule Moshi, nilijiuliza hivi kule Moshi magari yote ya polisi ni mazima?”.
“Nawashauri viongozi wote serikalini waige mfano wa Mkuu wa Mkoa Mh.PAUL  MAKONDA”.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE