November 30, 2017

USIKU WA DKT. SHIKA “900 ITAPENDEZAA” WAJA, KUFANYIKA DAR. LIVE MBAGALA DESEMBA 9/2017


1
Meneja wa Dk Shika Bi Kahabi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtambulisha Dk Louis Shika kulia  kwa wanahabari alipokuwa akitangaza Hafla ya Usiku wa USIKU WA 900 ITAPENDEZAA kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo.
2
Dk Louis Shika kulia  akijitambulisha  kwa wanahabari alipokuwa akitangaza Hafla ya Usiku wa USIKU WA 900 ITAPENDEZAA kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo.
…………………………………………………………………………………
Usikuwa 900 itapendeza, ni hafla maalum ya Kumtambulisha DrLuis Shika kama miongoni mwa watu waliopata umaarufu mkubwa kwa muda mfupi lakini pia kumpongeza kwa kushinda mnada wa nyumba za Tajiri Lugumi, na kumuweka rasmi kwenye muonekano mpya wa ubilionea.ambapo Vilevile Dr.Shika ataongea historia yake alipotoka na mpaka hapa alipo kwa sasa .
Halfa hii inatarajiwa kufanyika usiku wa tarehe 9.Disemba 2017 katika ukumbi wa Dar Live Mbangala jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na zaidi ya  watu 5000, huku hafla hii ikisindikizwa na bendi mbalimbali ikiwemo Twangapepeta, Jahazi Modern Taarab pamoja na Wasanii wa bongo fleva, wakiwemo wasanii wachekeshaji kama vile MC Pilipili.
Mbali na hivyo, kutakuwa na Mgeni rasmi ambaye ataifungua hafla hiyo, huku akitambulishwa pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Group Bw.Erick Shigong kama mtu aliyechangia kwa namna moja ama nyingine kumfanya Dr.  Shika kuonekana mtu katika watu kupitia Global tv.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE