November 22, 2017

UFUNGUZI WA KITUO CHA KISASA CHA KUTOA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU,UKIMWI NA MAGONJWA YATOKANAYO NA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kwenye hospitali ya Magonjwa ya kuambukiza Kibong’oto Mkoani Kilimanjaro,kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anna Mghirwa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna mghirwa akiongea  wakati wa ufunguzi wa kiyuo hicho ambacho kitakuwa kikihudumia wachimbaji wa madini na familia zao kutokana na kifua kikuu na kudhurika na magonjwa ya mfumo wa hewa
Baadhi ya wachimbaji wa madini kutoka Mererani ambao walishiriki ufunguzi wa kituo hicho
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Kibong’oto wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu(hayupo pichani)wakati akihutubi ambapo alisema kituo hicho ni miongoni mwa vituo 11 vilivyojengwa katika nchi 10 za SADC
 Waziri wa Afya pamoja na viongozi wa Mkoa,Mbunge pamoja na wadau wa madini wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo hicho
 Waziri Ummy Mwalimu(wa kwanza kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghirwa(kulia) walikagua chumba chenye mashine ya Uchunguzi (Xray) iliyofungwa kwenye kituo hicho
Waziri wa Afya (katikati)akimsikiliza kwa makini bw.Athumani Abdalah(hayupo pichani)wakati akitoa ushuhuda wake kama mchimbaji mdogo mdogo,kishoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghirwa na kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Siha Dkt.Godwin Mollel
……………
Na.Catherine Sungura,WAMJW,Siha
 Shughuli za uchimbaji madini duniani kote zinatambulika kama ni shughuli hatarishi kwa afya ya binadamu kutokana na urahisi wa kudhurika pia athari kwenye afya ya mapafu kutokana na vumbi zito
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma za Kifua Kikuu,Ukimwia na Magonwa yatokanayo na shughuli za uchimbaji madini katika hospitali ya magonjwa ya kuambukiza Kibong’oto iliyopo Mkoani Kilimanjaro
Waziri Ummy amesema shughuli za uchimbaji humuweka mchimbaji kwenye hatari zaidi ya kupata kwa urahisi ugonjwa wa Kifua Kikuu na Magonjwa mengine sugu ya mfumo wa njia ya hewa,vile vile shughuli za kijamii,kiuchumi na kiutamaduni katika maeneo ya migodi zimekua zikichochea kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika maeneo hayo.
“Kutokana na changamoto hizi na ili tupunguze tatizo LA Kifua Kikuu na UKIMWI katika sekta ya madini,mwaka 2015 nchi kumi za SADC kwa pamoja ziliomba fedha katika mfuko wa Dunia wa Kudhibiti magonjwa ya UKIMWI,Kifua Kikuu na Malaria(Global fund ATM) ili kukabiliana na tatizo hili katika sekta ya madini”(TB in the Mining Sector(TIMS)
Aidha,alisema tangu kuanza kutekelezwa kwa mradi huo Januari,2016,tayari matokeo ya utafiti zilizofanyika maeneo ya migodi yameonesha kuwepo kwa kiwango kidogo cha ufahamu na uelewa wa masuala ya Kifua Kikuu,UKIMWI na magonjwa yatokanayo na shughuli za uchimbaji miongoni kwa wachimbaji na jamii inayowazunguka.
” wachimbaji wadogo wadogo wameendelea kuathirikanna vumbi LA silika kutokana na kutumia dhana duni za uchimbaji usiozingatia masharti ya udhibiti wa vumbi,licha ya sekta hii kuchangia kwa kiasi kikubwa pato LA Taifa,hali a upatikanaji wa huduma za afya kwenye migodi si ya kuridhisha”
Kituo hicho cha kisasa ambacho ni cha kwanza nchini kitakua mfano na kitasaidia kuokoa maisha na ulemavu utokanao na shughuli za uchimbaji kutokana sehemu zingine nchini,kimefungwa vifaa vya uchunguzi ikiwepo xray na kupatiwa daktari bingwa na wataalamu wa maabara na mionzi

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE