November 26, 2017

UCHAGUZI MDOGO UDIWANI LEO, POLISI IRINGA WAKAMATA WALIOTAKA KUHUJUMU UCHAGUZI KITWIRU IRINGA MJINI ,LUSINDE AMPA NENO MSIGWA NA MBOWE


UCHAGUZI mdogo  wa  udiwani  katika kata 43  nchini  unataraji   kufanyika  leo   huku kata ya  Kitwiru  katika jimbo la  Iringa  mjini wagombea  wawili  wa  Chama  cha  Mapinduzi (CCM)  Barakata  Kimata na  yule wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema)Bahati Chengula wakionyesha  mchuano  mkali   na kila  chama  kukituhumu  chama  kingene  kwa kucheza rafu katika kampeni za lala salama.
 
Mapema  majira ya  saa 4  asubuhi   jana Chadema  walieneza  taarifa  katika  mitandao  ya   kijamii  wakieleza  kulalamika  kuvumiwa  kwa  ngome  yao na  watu  wasiojulikana wakiwa na bastola na  kuondoka na kada  wake  mmoja  aliyetajwa kwa   jina la  Linus.
 
Taarifa   hizi  zilikanushwa  na  jeshi la  polisi  kwa madai  kuwa  kada  huyo wa Chadema  alikamatwa na  jeshi la  polisi  kwa  ajili ya mahojiano  baada ya  simu  yake  kutumia kusambaza  jumbe  mbali mbali mbali  zenye lengo la kuvuruga  uchaguzi  huo  wa  Kitwiru .
 
Alisema  kuwa  jeshi la  polisi  lilipata  taarifa  za  siri  kutoka kwa wasiri  wake  kuhusiana na mtandao  wa  vijana  kutoka nje ya  mkoa  wa Iringa na ndani ya  Iringa  ambao  wanaendesha zoezi la  kutaka  kuvuruga  uchaguzi huo na hata  kusambaza  jumbe  mbali mbali  za  vitisho  kwa  wananchi .
Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Julius Mjengi  akithibitisha  kukamatwa kwa  mtuhumiwa  huyo jana kwa  njia ya  simu  alisema  kuwa bado jeshi lake  linaendelea  kumhoji  mtuhumiwa  huyo  ambae  alikutwa na ushahidi  wa  jumbe  hizo  .
 
“ Watu  wanaendelea  kupotosha katika  mitandao  ya  kijamii kuwa  amekamatwa na  watu  wasiojulikana  huu ni upotoshaji huyu  amekamatwa na  polisi  na  tunamshikilia wakati  tukiendelea  kuwasaka  wenzake  ambao  wamekuja kutaka  kuvuruga  uchaguzi huu “
 
Wakati  huo  huo  jeshi la  polisi  mkoani hapa  limewataka  wananchi  wa kata ya  Kitwiru kutokuwa na  hofu yoyote na  kwenda kushiriki  uchaguzi  bila  kutishwa na mtu  kwani ulinzi  umewekwa  kuona  wananchi  wote  wenye sifa  wanashiriki  zoezi hilo  bila kufanyiwa  vurugu na  mtu  yeyote .
 
Ndani ya  mkoa wa Iringa  uchaguzi  huu  mdogo wa  udiwani  unafanyika  leo katika kata mbili kati ya  Kimala  wilaya ya  Kilolo  ambako  diwani wake wa CCM alifariki  dunia na kata ya Kitwiru  ambayo  diwani  wake wa Chadema alijiuzulu na  kujiunga na CCM na  ndie  anayegombea  kupitia CCM .
Vyama  ambavyo vilijitokeza  kusimakisha  wagombea kwenye kata   ya  Kitwiru ni NCCR Mageuzi, Chadema, CUF, ACT Wazalendo na CCM na ADC  wakati  vyama  vilivyofanya kampeni  ni  vitatu  pekee CCM , CUF na  Chadema na  vingine vilishindwa  kabisa  kufanya kampeni  kutokana na ukata .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE