November 15, 2017

TSSF YAFUNGIWA NA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inapenda kuujulisha Umma kuwa imesimamisha shughuli za Shirika la TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION (TSSF) kuanzia tarehe 14/11/2017 ili kupisha uchunguzi unaofanywa dhidi ya tuhuma za Shirika tajwa kutapeli watu mbalimbali nchini kwa kisingizio cha kuwapatia mikopo kwa ajili ya elimu ya juu kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Kwa taarifa hii uongozi wa Shirika unaagizwa kusimamisha shughuli zake zote ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi zote za shirika hadi uchunguzi utakapokamilika. Aidha, viongozi wa shirika wanaagizwa kufika katika Ofisi ya Msajili wakiwa na nyaraka halisi za usajili wa Shirika (Cheti na Katiba) kabla ya tarehe 21/11/2017.
  1. S. Katemba
MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)
14/11/2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE