November 3, 2017

TAASISI YA UZALENDO YAUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA WIZI WA KAZI ZA WASANII

1
Steve Nyerere amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe kwa kazi wanayofanya na jinsi wanavyokemea na kusisitiza ili kukomesha wizi wa kazi za sanaa nchini wakitoa wito  kwamba wasanii wanatakiwa kula jasho lao na si kuibiwa na kuneemeka watu wengine badala ya wasanii wenyewe ambao ndiyo wenye kazi na wanaotoa jasho katika kutengeneza kazi hizo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Uzalendo Tanzania Bw. Steven Mengele aka Steve Nyerere akizungumza katika mkutano na wasanii wenzake wakati walipokutana leo wakati alipopongeza na  kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Kampuni ya Msama Auction Mart kupitia Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama katika mapambando dhidi ya wizi wa kazi za sanaa ambazo zimekuwa zikirudufiwa na kuuzwa bila Stika za TRA na Makubaliao ya wasanii ambao ndiyo wenye kazi zao hivyo kuwanyonya wasanii.
Amesema Taasisi hizo ya Uzalendo pamoja na wanachama wake wanaunga mkono vita hiyo na wataunganisha nguvu katika  mapambano ya kuwakamata wezi wa kazi zao mpaka wizi huo ukome mara moja na wasanii kuanza kunufaika na kazi zao, Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Breakpoint Kinondoni jijini Dar es salaam
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart  Bw. Alex Msama akiwashauri wasanii kutengeneza kazi zenye kiwango ili waweze kupata soko zuri hapa nchini huku akiwaambia Msiegemee kwenye Filamu za Mapenzi tu kuweni wabunifu na kutengeneza filamu zenye maudhui mbalimbali ya kitanzania mtapata soko zuri sana tu haiwezekani filamu zenu zote zielezee mapenzi tu kuna mambo mengi mnaweza kufanya kuliko mapenzi peke yake.
4
Picha mbalimbali zikionyesha wasanii wa filamu waliohudhuria katika mkutano huo.
5 6 7

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE