November 2, 2017

SERIKALI YAYAAGIZA MAKAMPUNI KUWAJIRI WATANZANIA

IMG_3794
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali imeyaagiza makampuni ya Bima hapa nchini kuhakikisha yanaajiri watanzania badala ya sasa kuajiri wageni kutoka nje ya nchi ambapo ni makampuni matano tu hapa nchini yanaendesha bima ya maisha kati ya makampuni 31 yaliopo nchini huku mengi yakiwa ni kutoka nje ya nchi.
Akifungua mkutano wa Taasisi za bima kutoka nchi 20 za bara la Afrika(African Insuarence Organization) Naibu waziri wa Fedha Dkta Ashatu Kijaji aliwaambia washiriki kuwa serikali ya Tanzania kwa sasa imejikita kwenye uchumi wa viwanda na mchango wa sekta hiyo unahitajiki kufikia malengo tarajiwa ya kukuza uchumi.
Ameagiza sekta hiyo kuangalia upya muundo wa bima ya maisha ilikuweza kuendana na sera za nchi hususani ya viwanda bila kusahau kilimo itakayosaidia watanzania wengi kukuwa kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi ambapo pia amewataka kufanyakazi zaidi kuongeza wigo wa ongezeko la wananchi wanaojiunga na Bima ya maisha hapa nchini.
“Nimatarajio yangu kuwa sekta ya bima hapa nchini itasaidia ukuaji wa kiuchimi kwa wananchi kuweza kujiunga kwa wingi na hili natajia kwa siku mbili mtakazokaa hapa mtajadili ni namna gani mtaweza kuisaidia serikali kuweza kukuza uchumi hususani wa viwanda kwa malengo mtakayojiwekea”alisema Dkta kijaji
Kwa upande wake Kamishna wa Bima hapa nchini Baghayo Saqware amewambia kuwa wananchi wengi wanahitajika kuanzisha uwakala wa bima ilikuwezesha kukuwa kwa sekta hiyo ambayo wageni ndio wenye makampuni mengi kuliko wazawa hivyo ni fursa adhimu kwani vigezo vya kuanzisha uwakala vinalingana na sifa za watanzania wengi wa chini.
Akawataka Watanzania kutumia nafasi hiyo kuweza kujiunga na bima ilikuweza kujinufaisha kiuchumi kwani sekta hiyo itawasaidia kuweza kukopeshwa fedha na mabenki bila kuhitaji kuweka bondi au dhamana ambazo wamekuwa wakiwekeza kwa sasa kwenye taasisi hizo za kifedha.
Dkta Saqware  amesema kuwa sekta hiyo ni muhimili wa ukuaji wa uchumi ndio maana wameweza kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi na wao wamechukua maagizo ya Naibu waziri wa Fedha kama changamoto ya kukuza sekta hiyo hapa nchini.
Ambapo amewataka wananchi kuanza kufikiria mitazamo yao kujiunga na bima ya maisha ambayo kwao ni uwekezaji,kujikinga na madhara na mkombozi wa familia zao pindi wanapopata maafa mbali mbali.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE