November 23, 2017

SENEGAL VINARA AFRIKA KATIKA ORODHA MPYA YA VIWANGO VYA FIFA


Senegal imepanda hadi nafasi ya 23 kutoka 32 katika orodha ya shirikisho la soka duniani Fifa mwezi Novemba.
Pia wamepanda juu ya Tunisia na Misri na kuwa taifa linaloorodheshwa katika nafasi ya kwanza Afrika.
Hatua hiyo inajiri baada ya Simba hao wa Teranga kushinda mechi mbili dhidi ya Afrika Kusini mnamo mwezi Novemba hatua iliowafanya kufuzu katika kombe la dunia mwaka ujao nchini Urusi.
Nigeria ndio inayoorodheshwa ya chini miongoni mwa mataifa yaliofuzu katika kombe la dunia katika mataifa hamsini duniani na manane kutoka Afrika.
Burkina Faso ndio waliopiga hatua kubwa barani Afrika baada ya kupanda nafasi 11 juu na kufikia nafasi ya 44 duniani na sita katika bara Afrika.
Mataifa yanayoongoza katika orodha hiyo ya Fifa duniani ni Ujerumani, Brazil, Ureno, Argentina na Ubelgiji.
  • 1.Senegal (23)
  • 2.Tunisia (27)
  • 3.Egypt (31)
  • 4.DR Congo (36)
  • 5.Morocco (40)
  • 6.Burkina Faso (44)
  • 7.Cameroon (45)
  • 8.Nigeria (50)
  • 9.Ghana (51)
  • 10.Ivory Coast (61)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE