November 3, 2017

SEKTA YA BIMA YATAKIWA KUAJIRI WATANZANIA

 
Kampuni za Bima nchini zimetakiwa kuajiri watanzania badala ya
mfumo wanayotumia kwa sasa ambapo makampuni mengi yamekuwa yakiajiri
wafanyakazi wao kutoka nje yanakotoka, pia sekta hiyo ya bima imeagizwa kuwekeza
mitaji yao katika viwanda kuendana na sera nchi ya uchumi wa kati na viwanda.

 Naibun waziri wa Fedha Dkt Ashantu Kijaji akiongea wakati wa kufungua semina ya wadau wa sekta ya Bina
inayofanyika jijini Arusha.

 Baadhi ya wadau wa sekta ya Bina kutoka nchini za Afrika wakisikiliza hotuba ya mgeni
rasmi (hayupo pichani) alipokuwa akiongea.

 Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro akimwakilisha  mkuu wa mkoa wa Arusha
Gambo ambaye hakuwepo.

 Kamishina wa Bima Saqware akiongwa wakati wa hotuba ya
 ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mapema leo.

 …………………………………………………………………
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Fedha Dkt Ashatu Kijaji
alipokuwa akifungua Semina ya siku mbili ya wadau wa Bima kutoka nchi 20 barani
Afrika (African Insurance Organization) semina inayofanyika jijini Arusha
ambapo amewaagiza wadau wa sekta hiyo kote afrika kuangalia ni njia gani zitumike
kusaidia serikali za Afrika kuweza kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.
 
Sera ya serikali ya inayoongozwa na Rais John
Pombe Magufuri ni nchi kufikia uchumi wa kati, hii haitaweza kufanikiwa iwapo
kila mmoja wetu hataweza kufanyakazi ikiwemo kupunguza tatizo la ajira hapa
nchini nanyi ni wadau wakubwa na mna nafasi kubwa ya kuongeza wigo wa kupunguza
tatizo hilo”
 aliongeza
Dkt Kijaji.
 
Ameongeza kuwa maeneo mengi ya kiuchumi yanahitaji mitaji
ikiwemo Afya kwenye jamii, Kilimo na ufugaji, hivyo sekta ya bima inaweza kuwa
ni  muhimili mkubwa kufikia maendeleo,
kwani imekuwa ikiwagusa wananchi wengi,
“mna wajibu wa
kuongeza wigo na wanachama wenu kuweza kupata mitaji ya uwekezaji”
 
Kwa upande mwngine Kamishna wa Bima hapa nchini Dkt.Baghayo
Saqware amesema kuwa watanzania wengi bado hawajajiunga na bima ya maisha kwa
kutokujua faida zake ikiwemo ya kujikinga na majanga, uwekezaji na kuondoa
familia zao kwenye hofu pindi wanapopatwa na maafa mbali mbali kwenye maisha
yao ya kila siku.
 
Amesema kuwa lengo lao kubwa ni kuweza kuifikia jamii kubwa na
kuwa wadau wakubwa wa uwekezaji hapa nchini kama zilivyo taasisi nyingine za mifuko
ya hifadhi za jamii na kuwaondoa hofu wale wasiojua faida za Bima waweza
kuchukua hatua sasa za kujiunga iliwawe wanachama.
 
“Wananchi wengi bado hawana ufahamu na kujua faida za
kujiunga na bima ila tunafanya kazi ya utoaji wa elimu kuweza kuwafikia wananchi
wengi hususani Wafanyabiashara wadogo, Wafugaji, Wakulima na wananchi wa vipato
vya chini hii itasaidia kuongeza mitaji itakayowasaidia uwekezaji mkubwa hapa
nchini katika kufikia uchumi wa kati”
alisema Dkt.Saqware

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE