November 24, 2017

SAMIA KUZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI


NO EXCUSE 4
Kaimu mkurugenzi wa shirika la wanawake katika Sheria  na Maendeleo Afrika (WiLDAF),Anna Kulaya,akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kampeni hizo
No EXCUSE 1
Afisa Mawasiliano kutoka TBL,Amanda Walter akiongea wakati wa mkutano wa  waandishi wa habari kihusu kampeni hizo
NO EXCUSE 6
Baadhi ya wadau wa Masuala ya kupambana  na vitendo dhidi ya ukatili katika picha wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam
NO EXCUSE 7
Baadhi ya wadau wa masuala ya kupambana na vitendo dhidi ya ukatili wa kijinsia katika picha ya pamoja baada ya kufanya mkutano wa waandishi wa habari
……………………………………………………………………….
Kampeni  ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia inayoshirikisha wadau mbalimbali wanaopinga  vitendo hivyo inazinduliwa  nchini kesho jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais,Mh.Samia Suluhu Hassan, anatarajia kupokea maandamano ya wadau hao ambayo yataanzia katika viwanja vya shule ya msingi ya Muhimbili na kuishia katika viwanja vya leaders.
Kampeni hizo ambazo hufanyika duniani kote kwa hapa nchini zinaratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la wanawake katika sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) kwa kushirikiana na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) ,Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia
Mwaka huu kampuni ya Tanzania Breweries Limited,TBL chini ya kampuni mama ya ABINBEV imejitosa katika kampeni hizo ambazo itasambaza jumbe mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kampeni yake ya #NO EXCUSE!!! ACHA SABABU, BADILIKA inayoenda sambamba na kampeni yake ya kuelimisha jamii juu ya Unywaji wa kistaarabu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE