November 4, 2017

SAMAKI WA AJABU WABAINIKA HIFADHI YA PORI LA AKIBA ZIWA RUKWA
Na Elizabeth Ntambala ,Mtukiodaimablog Rukwa 
Hifadhi yà pori la akiba la uwanda lililopo katika mwambao Wa Ziwa Rukwa wilaya ya sumbawanga mkoani Rukwa imetangaza kuwepo Kwa samaki Wa aina yake wasiopatikana popote duniani. 

Meneja Wa pori la akiba la uwanda Mark Chuwa amesema hayo katika kikao cha Pamoja baina yà Mkuu Wa mkoa Joachim Wangabo na wakuu Wa mashirika yà umma yaliyopo mkoani Rukwa. 

Chuwa alisema Ziwa Rukwa lina samaki Wa aina yake wasiopatikana sehemu yoyote duniani wanaofahamika Kwa jina la Oreochromis rukwaensis ambao ni maarufu mkoani Rukwa Kwa jina la Magege wenye ladha mzuri. 

Pamoja na kuwepo Kwa     jukumu la uwingi walilo nalo kama wahifadhi wametakiwa kuhakikisha mazingira ya mazalia ya samaki hao yamebaki salama wakati wote ili samaki hao wasipoteze kizazi kutokana na uvuvi haramu ulioshamiri Ziwa Rukwa. 

Chuwa alidai kuwa changamoto kubwa ya uvuvi haramu katika Ziwa Rukwa inatishia uhai Wa samaki hao kiasi kwamba wameingizwa katika orodha ya viumbe walioko hatarishi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE