November 19, 2017

RAIS MAGUFULI KUZINDUA KAMPENI YA UZALENDO TANZANIA

PIX 1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza jana Jijini Dar es Salaam na Wakuu wa Taasisi za Serikali kuhusu Kampeni ya Uzalendo  na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
PIX 2
Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali  Bw. Geofrey Mwambe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) (aliyesimama )akizungumza wakati wa kikao  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison  Mwakyembe pamoja na Wakuu hao kuhusu Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kuzindiliwa mwezi ujao Mjini Dodoma.
PIX 3
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiwaonyesha Wakuu wa Taasisi za Serikali Jarida la Nchi Yetu linaloelezea mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Tano  lililondaliwa na Idara yake kwa kushirikiana na Taasisi hizo jana Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo imeandaa Kampeni ya “Uzalendo na Utaifa” inayotarajiwa kuzinduliwa Disemba nane mwaka huu Mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lengo ikiwa ni kurejesha  hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza katika Taifa letu.
Akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Serikali jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Kampeni hiyo inadhamiria kuwakumbusha watanzania Utamaduni wetu na Uzalendo uliokuepo  miongoni mwa Watanzania ambao ulileta heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
“Kampeni hii ina lengo la kurudisha Uzalendo tuliokuwa nao Watanzania katika kuheshimu mali za Umma, kuogopa rushwa,ubaguzi wa kidini,kikabila,kiitikadi na kikanda  ambavyo vilianza kupotea,lakini Serikali ya awamu ya Tano imeanza kurudisha hivyo sisi kama watanzania tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi”Alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Kampeni hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya ikiwemo kurejesha na kuimarisha moyo wa Uzalendo na Utaifa kwa Watanzania hususan vijana na watoto umuhimu wa kuipenda na kuithamini nchi yao pamoja na kuimarisha umoja upendo na mshikamano wa kitaifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geofrey Mwambe amesema Taasisi za Serikali zinaunga mkono Kampeni hiyo kwani itasaidia watanzania wengi kuelewa historia na Utamaduni  ya nchi yao na kuitilia maanani popote watakapokuwa.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu “Nchi Yangu Kwanza” itakuwa ni endelevu na inatarajiwa  kufanyika kila mwezi Oktoba kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa  Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE