November 2, 2017

RAIS AAGIZA KURUDISHWA KWA HUKUMU YA KIFO

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ametaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo nchini mwake kwani watu wanacheza na maisha ya watu kwa kuua wenzao.
Rais Mugabe ametoa taarifa hiyo alipokuwa kwenye mazishi ya mwanasiasa mwenzake mjini Harare, na kusema kuwa sheria ya kunyongwa irudishwe kwani watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao.
“Acha turudishe hukumu ya kifo, watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao, hivi hii ndio sababu ya kuikomboa nchi? Tunataka nchi hii iwe ya amani na furaha, sio nchi ambayo watu wanauana”, amenukuliwa Rais Mugabe.
Taarifa zimeendelea kueleza kwamba kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ya Waziri wa Sheria kusema kuwa zaidi ya watu 50 wameomba nafasi ya kazi ya kunyonga watu mwezi uliopita.
Tukio la mwisho la kunyongwa mtu hadi kufa nchini humo lilikuwa mwaka 2005 baada ya mtu aliyekuwa akifanya kazi ya kunyonga kustaafu, ambapo mpaka sasa zaidi ya wafungwa 90 wapo wanasubiri hukumu ya kifo.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE