November 1, 2017

RAILA ODINGA ASEMA HATAMBUI UCHAGUZI WA UHURU KENYATTA

   

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
                                     Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa Raila Odinga ameapa kuendelea kufanya maandamano dhidi ya uchaguzi wa Uhuru Kenyatta akisisitiza kuwa upinzani haumtambui.
Odinga anasema kuwa Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya baadhi ya makamishna katika tume hiyo.
Odinga ambaye alikuwa akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee.
Anasema kwamba iwapo uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote.
Mr Odinga pia amesema kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na demokrasia ilipatikana.

Amesema kuwa iwapo uchaguzi wa Uhuru utaruhusiwa kuna uwezekano kwamba ataingilia katiba na kuongeza muhula wa kuongoza.

''Tutaendelea kufanya maandamno kila mara'', alisema Raila Odinga.
Rais Uhuru Kenyatta baada ya kutangazwa mshindi
                                     Rais Uhuru Kenyatta baada ya kutangazwa mshindi
Bwana Odinga alisusia uchaguzi wa marudio wa urais wiki iliopita kwa sababu anasema kuwa hakuna mabadiliko yaliofanyiwa tume ya uchaguzi ya IEBC baada ya mahakama ya juu kupata makosa na ukiukaji mkubwa wa katiba.

Watu waliojitokeza kupiga kura ni chini ya asilimia 39.
Ametangaza kuwa atazindua bunge la wananchi ambalo litashirikisha jopo litakalochunguza kufeli kwa tume za uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE