November 1, 2017

NDELE MWASELELA ATOA SOMO KWA WADAU WA ELIMU

NA EZEKIEL KAMANGA -matukiodaimablog 
Mdau wa Elimu nchini Ndele Mwaselela amewataka wananchi wa Kata ya Iyela waache kuzaa kama hawataki kujenga shule ya Iyela. 

Ameyasema hayo katika mkutano na wa hadhara baada ya kusikitishwa na msongamano wa watoto darasani huku wazazi wakishidwa kukamilisha madarasa. 

Shule ina upungufu wa madarasa 13.Ndele amechukizwa na hatua ya wazazi na wadau na wawekezaji mbalimbali kushindwa kuchangia madarasa hivyo kuwataka wazazi wakamilishe haraka ili wapige mbao yeye atatoa mabati yote ya kukamilisha madarasa hayo.

Hata hivyo Ndele ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi Kata ya Iyela kwani amesema hatavumilia mapatano nyumbani na kwamba wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. 

Aidha amekabidhi fedha za ulinzi jumla ya shilingi laki mbili kwa shule ya Iyela na shilingi laki tano kwa shule ya Msingi Ilangali ya Kata ya Nsenga iliyopo Mbeya vijijini. 

Kwa  upande wa wazazi Furaha Mwankuga amesema Ndele Mwaselela anapaswa kuungwa mkono na wazazi wote na msaada wake uhamasishe wazazi kuchangia shule hiyo badala ya kusubiria msaada. 

Pia Mwankuga amewapongeza walimu kwa juhudi kubwa ambapo kati ya wanafunzi 190 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu ni wanafunzi kumi na tatu tu ndiyo wamekosa ufaulu. 

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Iyela 
Anna Mbela amesema wanafunzi sita wamepata alama A hivyo kuifanya shule ya Iyela kuwa ya nane Kiwilaya ambapo Ndele amesema atawaomesha wanafunzi wote wa Kata ya Iyela waliopata alama A. 

Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Iyela Dickson Sinkwembe amesema wazazi wawahimize watoto kuzingatia masomo badala ya kuwaachia mzigo walimu pekee. 

Anna Sipalika Mtendaji wa Kata amesema wazazi wote ambao hawatawahimiza watoto shule na watakaowakatisha masomo kwa ujauzito watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

 Shule ya Iyela kwa sasa imepiga hatua katika taaluma kutokana na kwenda na wakati ambapo ina darasa la computer ambalo lilifadhiliwa na Ndele Mwaselela.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE