November 3, 2017

NAPPE ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU KUSALIA AU KUONDOKA CCM

Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye amefunguka kutokana na tetesi zilizokuwa zikizagaa na kuzungumzwa kuwa naye yuko mbioni kuhama chama chake cha mapinduzi kama ambavyo amefanya Lazaro Nyalandu.
Nape kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter amepost picha ambayo wako watatu akiwemo yeye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge wa Singida kupitia CCM ambaye amejivua uanachama , Lazaro Nyalandu.
Baada ya kuweka picha hiyo Mh. Nnauye ameandika maneno ambayo yanaonesha hana mpango kabisa wa kuhama chama chake kama ambavyo inahisiwa na watu mbali mbali.
“Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani. Siamini sana katika kubadili imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani na sio nje!” Ameandika Nape
Kufuatia Mh Nape Nnauye kuonesha msimamo wake huo, hatua hii moja kwa moja itafunga majadiliano ya watu katika sehemu tofauti kuwa ana mpango wa kukitosa chama cha CCM.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE