November 27, 2017

MREMBO WA AFRIKA KUSINI ASHINDA TAJI LA MISS UNIVERSE 2017

Mrembo, Nel-Peters.
NEL-PETERS (22) mrembo aliyeshika nafasi ya kwanza nchini Afrika Kusini amevishwa taji la Mrembo wa Dunia (Miss Universe 2017) akiwashinda Miss Colombia, Laura Gonzales (mshindi wa pili) na Miss Jamaica, Davina Bennett (mshindi wa tatu) katika mchuano uliofanyika jana Jumapili jijini Las Vegas, Marekani.
Mrembo huyo ametunukiwa taji hilo ambapo pia hivi karibuni alitunukiwa shahada katika menejimenti ya biashara kwenye Chuo Kikuu cha North-West cha Afrika Kusini. Akihojiwa wakati wa mashindano hayo, Nel-Peters ambaye ni mzaliwa wa Western Cape nchini humo, alisema kuna wakati aliwahi kutishwa kwa kushikiwa bunduki na watu ambao hakuwataja, akaongeza kwamba tukio hilo limemfanya kuwa na mpango wa kuwafundisha wanawake jinsi ya kujilinda.
Akijibu maswali zaidi, mrembo huyo alisema suala kubwa zaidi kwake linalomkera ni wanawake kulipwa asilimia 75 ya mshahara kwa kazi ileile ambapo wanaume hulipwa asilimia 100. “Kuna sehemu za kazi wanawake hulipwa asilimia 75 kwa kazi ileile, saa zilezile za kazi wafanyazo wanaume. Sidhani kama hii ni haki, lazima tuwe sawa duniani kote,” alisema Nel-Peters.
Washindi 13 walioingia fainali walitoka nchi za Thailand, Sri Lanka, Ghana, Hispania, Ireland, Croatia, Uingereza, Marekani, Brazil, Canada, Philippines, Venezuela na China.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE