November 29, 2017

MPANGO WA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA KUJA

0001
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika kongamano lasiku mbili la kisayansi lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuwahusiha wataalamu mbalimbali wa afya. Naibu waziri huyo ameipongeza MNH kwa kuboresha huduma za afya zikiwamo za kupandikiza figo na upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wasiosikia.
0002
Wataalamu wa afya wa Muhimbili pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye kongamano hilo leo.
0003
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Laurence Museru akitoa mada kwenye kongamano hilo leo.
0004
Baadhi ya wataalamu wa afya wakifuatilia kongamano hilo leo.
0005
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu mbalimbali wa afya leo.
……………….
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili
……………..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile  leo amefungua kongamano la Kisayansi la Hospitali ya Taifa Muhimbili  na kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kutoa muongozo mpya wa matumizi  ya dawa ili kudhibiti matumizi holela ya dawa.
Amesema muongozo huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya dawa ambayo yanachangia usugu wa dawa katika mwili wa binadamu.
“Muongozo huu mpya utakapotolewa utatumika  katika Hospitali zote nchini na pia serikali tayari imeoredhesha dawa muhimu na dawa hizi zinapatika kwani serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shiling bilioni 30 hadi kufikia bilioni 269,” amesesisitiza Dkt. Ndugulile.
Pia, Naibu Waziri Ndugulile ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha inapunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Muhimbili tayari imeanza kutoa huduma ya kupandikiza figo, kufanya upasuaji wa kuwawekea vifaa vya kuwasaidia watoto kusikia na sasa wataalam wengine wanajiandaa kwenda India ili kujengewa uwezo wa kufanya upasuaji wa kupandikiza Ini.
“Nimefurahishwa  sana na mipango mikakati mliyojiwekea  na kutoa huduma za kibingwa za juu hapa nchini , baadhi zikiwa za kwanza kwenye sekta ya Umma hata kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki  hasa upandikizaji wa vifaa vya kusikia na figo,’’ amesema Naibu Waziri.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema  pamoja na changamoto mbalimbali hospitali hiyo inaendelea kuboresha huduma zake na tayari imeongeza mashine za kuchuja damu kutoka 17 hadi 42, vyumba vya upasuaji  kutoka 13 hadi 20 pamoja na kuongeza  vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka 21 hadi 88.
Kongamano hilo la Kisayansi ni la kwanza kufanyika MNH ambalo limebeba mada kuu inayosema  changamoto na fursa za utoaji tiba nchini.
Mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo magonjwa ya Figo ,  Upandikizaji Figo na  Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE