November 21, 2017

Mahakama yaidhinisha ushindi wa Kenyatta Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Amollo Odinga
 
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Amollo Odinga
Kusherehekea
Kusherehekea uamuzi wa mahakama Nairobi
Mpiga picha wetu Peter Njoroge alipiga picha hizi za wafuasi wa Bw Kenyatta

wakisherehekea karibu na majengo ya Mahakama ya Juu, Nairobi baada ya majaji kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba.
Furaha
BBC
Kufurahia

Mahakama ya Juu Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimewasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio, yaidhinishwa ushindi wa Kenyatta.
  1. Mahakama ya Juu Kenya imeamua uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika tarehe 26 Oktoba, 2017 ulikuwa halali.
  2. Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kususia uchaguzi huo.
  3. Mahakama ya Juu ilikuwa imebatilisha uchaguzi wa kwanza uliokuwa umefanyika tarehe 8 Agosti ambapo Kenyatta alikuwa pia ametangazwa mshindi.

Maandamano ya ghasia yafanyika ngome za upinzani Kenya

Uamuzi wa mahakama ya juu wa kuidhinishwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Oktoba 26 umezua maandamano ya ghasia katika maeneo yanayodaiwa kuwa ngome za upinzani nchini Kenuya.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation wafuasi wa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga waliandamana ili kuonyesha kutoridhishwa kwao na uamuzi huo.
Maandamano hayo yalibadilika na kuwa ya ghasia katika maeneo kadhaa ya Nyanza, nyumbani kwa Odinga , katika maeneo ya Kibira na Mathare mjini Nairobi.
Mjini Kisumu, gari moja la kibinafsi lilichomwa katika eneo la Kondele muda mfupi baada ya ghasia kuzuka katika mji huo wa ziwa Victoria kufuatia uamuzi huo wa mahakama.
kulingana na gazeti hilo vijana walifunga barabara zinazoelekea mjini Kisumu kwa kuchoma magurudumu ya gari na mawe.
Waliwazuia watu watatu waliokuwa katika gari hilo la kibinafsi , wakawapiga na kuwaibia kabla ya kuliharibu gari hilo na kulichoma.
Watatu hao walikimbilia katika kituo cha polisi cha kondele wakihofia maisha yao.
Ghasia zilizokumba baadhi ya ngome za upinzani nchini Kenya baada ya uchaguzi wa  rais Uhuru Kenyatta Kuidhinishwa na mahakama ya Juu
Ghasia zilizokumba baadhi ya ngome za upinzani nchini Kenya baada ya uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta Kuidhinishwa na mahakama ya Juu
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amezungumzia kuhusu uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu wa kuidhinisha uchaguzi wa Uhuru Kenyatta.
Kulingna na gazeti la daily Nation, Bwana Odinga kupitia taarifa iliotolewa na mshauri wake Salim Lone, amesema kuwa serikali ya Jubilee sio halali akiongezea kwamba uamuzi huo wa mahakama ya juu ulifanywa kupitia shinikizo.
''Sisi watu wa Nasa tayari, tulikuwa tumeamua kabla ya uamuzi wa mahakama kwamba hatuitambui serikali ya Uhuru Kenyatta'', alisema.
''Uamuzi huo haujabadilishwa na uamuzi wa mahakama ya juu ambao haukutushangaza. Ni uamuzi uliotolewa chini ya shinikizo kubwa ,hatushutumu mahakama tunaihurumia''.
Ushindi wa rais Uhuru Kenyatta mnamo mwezi Oktoba 26 uliidhinishwa na mahakama hiyo kupitia uamuzi wa pamoja wa majaji sita wa mahakama ya juu.
Kulingana na gazeti hilo bwana Lone amedai kwamba mahakama ilikutana chini ya shinikizo kubwa, baada ya kushindwa kukutana kutokana na wasiwasi mkubwa wa kiusalama kufuatia kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa dereva wa naibu jaji mkuu kabla ya kusikizwa kwa kesi ya uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba.
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE