November 18, 2017

MACHAFUKO KENYA WATU WAUAWA KTK MAKARIBISHO YA RAILA

       Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kutoka Marekani                    Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kutoka Marekani                

Takriban watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa Nairobi huku maafisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga .
Gari moja la maafisa wa polisi pia lilichomwa .
Makundi ya watu yalikusanyika katika uwanja wa ndege kumkaribisha kiongozi huyo amabye alikuwa amerejea kutoka mataifa Marekani.
Raila Odinga alisusia marejeleo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Kulikuwa na ripoti za maafisa wa polisi waliorusha vitoa machozi katika gari la Raila Odinga alipokuwa akielekea mjini.
Siku ya Jumatatau Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta alibuka mshindi.

.............................................................................................................................................

Ili  uweze  kupata  habari zetu  kwa video ingia katika  chanel yetu ya  Yotube :matukiodaima kisha Suscriber   au pakua APP ya matukiodaima katika Play Store  

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE