November 2, 2017

MABENKI HAPA NCHINI YATAKIWA KUANGALIA VIWANGO VYA RIBA ZAO

image3
Mhe Gambo akizungumza na watumishi wa NMB na wateja waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMB Ngaramtoni
………….
Na Mahmoud Ahmad Arusha
 Serikali imeyataka mabenki hapa nchini kuangalia upya viwango vya riba zao wanazotoza wananchi ili kuweza kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kuweza kukopa hiyo itasaidia ukuaji wa pato la wananchi na kusaidia malengo ya serikali ya awamu ya Tano kuinua hali za wananchi wanyonge.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo ameyasema hayo wakati akizindua tawi la benki ya NMB katika mji mdogo wa Ngaramtoni. Mhe Gambo ameyashauri mabenki nchini kuona namna wanaweza kubadili matumizi ya fedha zao zinazolengwa kwa jamii yaani CSR (Corparate Social Responsibility) kwa kuangalia namna ya kuwainua watu wa hali ya chini kwa kuwakopesha fedha hizo pasi na masharti magumu ya dhamana.
“Nimefurahi kusikia NMB kwa mwaka huu pekee mmetenga kiasi cha Shilingi Bilioni moja na nusu kama sehemu ya CSR, sasa kwakua fedha hizo zimelengwa kwenda kwa jamii na benki inakua haina cha kupoteza sana kwa fedha hizo ninafikiria sasa muanze kuzitumia fedha hizo kutoa mikopo ya masharti nafuu na bila dhamana.” alisema Gambo.
“Watu wetu wanakua na shida ya mitaji midogo kama laki mbili ama tatu lakini akienda kwenye taasisi za kifedha ataambiwa apeleke hati ya nyumba ama kadi ya gari kitu ambacho hawezi kuwa nacho,sasa naona  zile fedha za CSR likazibe hili ombwe kwa kuwapatia wanyonge mikopo isyo ya masharti magumu ili kuwajengea uwezo wao wa kukopesheka kwa mikopo mikubwa zaidi.” Gambo alishauri.
Mkoa wa Arusha chini ya Mhe Gambo umekua ukijitahidi kuinua hali za wananchi wa kipato cha chini kwa kuwapatia mikopo mbalimbali ya nafuu, mathalani kwa mwaka huu zaidi ya vijana 200 walipatiwa mikopo ya pikipiki, ambapo fedha zitokanazo na marejesho yao zinakopeshwa kwa akina mama  500 kwa kupatiwa mikopo ya shilingi laki mbili  kila mmoja bila dhamana wala masharti yoyote.
Mafanikio katika miradi hii ndio inayomshawishi Mhe. Gambo kuwahakikishia benki ya NMB juu ya usalama wa fedha zao endapo wataliamini kundi hili na kulifikiria katika mikopo isiyo na dhamana ngumu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo (kulia) akiwa katika mazungumzo na wataalam toka benki ya NMB. Kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja wadogo na Kati, akifuatiwa na meneja wa kanda ya kati akifuatiwa na Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NMB

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE