November 21, 2017

MAAFISA WA TAASISI YA JK WAPIGWA MSASA NAMNA YA KUMPIMA MGONJWA UMEME WA MOYO


Picha no.1
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pal Bhadreshwara akionyesha namna  ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram – ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Picha no.2
Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijadili namna  ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram – ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Picha no.3
Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaonyesha wauguzi jinsi   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram-ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Picha no.4
Afisa Uuguzi kutoka  Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Deconne Jones akiwaeleza jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (Electrocardiogram – ECG) Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Danieli Yohana (katikati) na Mali Sabuni (kulia) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayofanyika JKCI.
Picha no.5
Afisa Uuguzi kutoka  Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Kiasha Munnis akifundisha jinsia   ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) kwa wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na wauguzi hao.
Picha no.6
Maafisa Uuguzi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia kwa makini maelekezo  ya  jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) wakati wa mafunzo ya siku tano ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) yanayotolewa na maafisa uuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.
Picha no.8
Mfunzo ya jinsi ya kumpima  mgonjwa umeme wa moyo (ECG) yakiendelea.  
Picha na JKCI

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE