November 21, 2017

LOWASA AZINGIRWA NA POLISI NYUMBANI KWAKE AKWAMA KWENDA KUMNADI MGOMBEA UDIWANI


Magari zaidi ya 10 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, yamezunguka nyumba ya Lowasa ambae ni waziri Mkuu mstaafu na kuzuia msafara wa Magari na pikipiki kuelekea kata ya Musa wilaya ya Arumeru kumnadi mgombea udiwani.
Tukio hilo limejiri leo majira ya saa 9 alasiri ambapo Polisi wenye silaha na mabomu walitanda nyumbani kwa Lowassa Monduli Arusha.
Aidha wafuasi wa CHADEMA waliomfuata kumpokea wakiwemo viongozi walizuiwa na Polisi huku Katibu Mwenezi wa Jimbo,John Seneu au Jombii akitiwa mbaroni na Polisi.
Kwa mujibu wa madai ya wafuasi wa CHADEMA wamedai kuwa, kitendo hicho kilichofanywa nanJeshi la Polisi kinachonyesha wazi kuwa ni hofu kwa CCM zinazopelekea kutumia vyombo vya dola vibaya.
   

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE