November 28, 2017

LIPULI FC KUWA MOJA YA TIMU BORA NCHINI

 TIMU ya soka ya LIPULI FC ya mkoani Iringa inakusudia kuwa miongoni mwa timu bora za soka nchini.

Akizungumza na wanahabari leo mkoani Iringa Katibu wa LIPULI FC Amon Ellias amesema timu yake kwa sasa ipo katika nafasi nzuri ktk msimamo wa ligi kutokana na juhudi ambazo uongozi ktk timu hiyo umekuwa ukichukua.

"Ukitazama msimamo wa ligi leo utaona nafasi ambayo timu yetu ipo na hiyo yote inakuonyesha juhudi madhubuti tunazochukua kama uongozi kwa pamoja"-Amon alisema.

Alisema moja ya mikakati ambayo inachukuliwa na uongozi ili kuipa timu mafanikio ni pamoja na kutafuta udhamini ili kuondokana na ukata wa fedha.

Amon alisema kwa sasa timu haina mdhamini hali ambayo sio nzuri sana kwa mustakabali wa timu.

"Kama ujuavyo soka la sasa ni lazima lichagizwe na fedha...nasi kwa kuliona hilo tunapambana usiku na mchana kuhakikisha tunapata fedha za kutosha kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu"-Alibainisha.

Aidha Amon aliitaja mikakati mingine ambayo ni pamoja na kuhakikisha timu inafanya usajili wa baadhi ya wachezaji ktk kikosi kama sehemu ya kujiimarisha zaidi.

Alisema kupitia dirisha dogo la usajili timu inakusudia kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ili kuwa na safu yenye makali kuliko ilivyo hivi sasa.

"Tumedhamiria kuimarisha safu ya ushambuliaji na tayari benchi la ufundi likiongozwa na kocha msaidizi Suleman Matola tayari wamekwisha tukabidhi sisi kama uongozi mapendekezo yao ya wachezaji wanaohitajika"-Alisema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE