November 27, 2017

KIMENUKA:AC MILAN YAMFUTA KAZI KOCHA MONTELLA ‘SASA NAFASI ANAIKAIMU GATTUSSO’

_98949320_14c95daa-b045-4d44-bf66-2f4f9a17bc19
Timu ya AC Milan imemtimua kocha Vincenzo Montella na badala yake imempa usukani Gennaro Gattuso kukisimamia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Klabu hiyo ipo katika nafasi ya 7 kwenye orodha kwenye ligi ya Serie A ikiwa na pointi 20, 18 nyuma ya mabingwa Napoli, baada ya ushindani wa ushindi mara mbili pekee wa ligi katika michuano yao ya nyuma.
Walitoka sare ya 0-0 na Torino nyumbani siku ya Jumapili na wameshindwa mechi zao 6 kati ya 14 msimu huu.
Gattuso, ambaye alikuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan anapokea wadhifa huo kutoka kuwa msimamizi wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 19 wa klabu hiyo.
AC Milan, ambao wameshinda taji hilo la Italia mara 18 na ni mabingwa mara 7 wa Ulaya, hawajawahi kuibuka katika nafasi tatu za juu katika ligi ya Serie A tangu 2013.
Wametumia pauni milioni 205 kuwasajili wachezaji wapya tangu mfanyabiashara wa kichina Li Yonghong kuidhibiti klabu hiyo Aprili mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE