November 15, 2017

KILICHOMUUA MUME WA ZAMANI WA UWOYA CHATAJWA

_98760336_cf957af6-2cc2-43d5-b087-f4ebed778434

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda Amavubi amefariki dunia,Ndikumana Hamad ‘Katauti’ alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mjini Kigali.Ndikumana alikuwa kocha msaidizi katika timu yake ya zamani ya Rayon Sports.Msemaji wa timu hiyo Olivier Gakwaya ameiambia BBC kuwa Katauti jana aliendesha mazoezi kama kawaida kabla ya kurejea nyumbani kwake mtaa wa Nyamirambo.”Baadaye hakujihisi vizuri akaenda kununua dawa katika duka la madawa lakini lakini hali yake imeendelea kuwa mbaya ndipo amepelekwa hospitali ya CHUK alikofariki,” amesema Oliver Gakwaya.Ndikumana alichezea timu ya Rayon Sports na timu ya taifa ya Rwanda kwanzia mwaka 1998 na kuwa nahodha wa muda mrefu wa Amavubi.
Pia alicheza soka la kulipwa ulaya katika timu za Gent na Anderlecht za Ubelgiji, Omonia Nicosia na Limassol za Cyprus.Mwaka 2009 alifunga ndoa na nyota wa filamu ya Tanzania Irene Uwoya maarufu Oprah kabla ya ndoa yao kuvunjika rasmi miaka 3 iliyopita.
Na alikuja kumalizia soka lake nchini Tanzania akiwa na klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ ya mkoa wa Shinyanga ndipo alipoamua kurudi nchini kwao

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE