November 6, 2017

KATIBU WA MADINI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA IDARA YA MADINI TANZANIA

Picha Na 1
Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila akizungumza na watumishi wa Idara ya Madini iliyo chini ya Wizara ya Madini (hawapo pichani) kwenye kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo Novemba 06, 2017
Picha Na 2
Sehemu ya watumishi kutoka Idara ya Madini iliyo chini ya Wizara ya Madini wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani)
Picha Na 3
Sehemu ya watumishi kutoka Idara ya Madini iliyo chini ya Wizara ya Madini wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani)
…………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila  leo tarehe 06 Novemba, 2017 katika Ofisi za Wizara ya Madini zilizopo jijini Dar es Salaam  amekutana na watumishi wa Idara ya Madini lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mikakati ya namna  ya  kuhakikisha kuwa  Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Profesa Msanjila aliwataka watumishi kufanya kazi yenye matokeo chanya kwa ubunifu wa hali ya juu ili sekta hiyo ichangie zaidi katika uchumi  wa nchi. Pia amewataka watumishi kuendana na  hali ya mabadiliko  yaliyotokea katika sekta hiyo.  Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuwasilisha  taarifa za utendaji kazi pamoja na changamoto zake. Wakati huohuo,  Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka  alimkaribisha Katibu Mkuu na kuahidi kutoa ushirikiano ili kuboresha utendaji kazi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE