November 21, 2017

HOT NEWS : MUGABE AJIUZULU URAIS ZIMBABWE

Katika dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .

Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habri cha reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya kesho Jumatano.

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.

Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.

Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.

Ameongoza kipindi cha uchumi ulioanguka ambapo raia wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980.

Hatua iliosababisha yeye kuanza kungatuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama ya kutaka mkewe kumrithi.

Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE