November 24, 2017

GARI LA HARUSI LAUA KUMI

Watu 10 wamefariki na wengine 24 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Hiace, kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Noah katika eneo la Ihuka wilayani Ikungi Mkoani Singida.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Toyota Hice T.581 BBV kulifuata gari aina ya Toyota Noah namba T.423 CFF na kusababisha vifo na majeruhi.

Kamanda Magiligimba amesema kuwa gari moja kati ya hayo lilikua linatokea kumchukua Bibi Harusi wakati gari nyingine ilikua inatokea kwenye msiba ndipo zilipokutana katika eneo hilo na kusababisha ajali ambayo taarifa za awali zinasema imetokana na uzembe wa dereva.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu Puma Singida, John Mmary amethibitisha kupokea Miili ya marehemu hao pamoja na Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walikua katika gari aina ya toyota Hiace na kuongeza kwamba majeruhi kumi na tano waliolazwa katika hopitali hiyo wanaendelea vizuri na matibabu isipokuwa wawili halizao siyo nzuri na wameumia sehemu kubwa za vichwa.
Magari yaliyo gongana aina ya Hice inadaiwa lilikuwa limewabeba maharusi pamoja na ndugu zao huku gari aina ya Noah ilikuwa imewabeba watu walio kuwa wakitokea kwenye msiba.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE