November 25, 2017

FAMILIA YAPATA UPOFU KATIKA MAZINGIRA TATANISHI


Mama mmoja aliyetambulika kwa jila la Doroth Otieno na watoto wake watatu wanaoishi Kisumu nchini Kenya, wamepata upofu wa ghafla bila kujua chanzo chake.
Doroth ambaye ameolewa na mkata miwa nchini Kenya, amesema hali hiyo imeleta matatizo kwenye ndoa yake na familia.
Akisimulia jinsi alivyopata upofu wake huo Doroth amesema mtoto wake wa kwanza nwenye miaka 16 na mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya wasichana ya Nyamonye, alipata upofu ghafla baada ya kuhisi kama macho yake yana mchanga, na kisha kuwa kipofu kabisa, huku watoto wake wawili wa kiume Vicent na Benson nao wakiwa na tatizo hilo hilo.
Mama huyo mwenye watoto watatu ameendelea kwa kueleza kwamba yeye mwenyewe siku moja baada ya kuamka na kuelekea zake sokoni ambako hufanya shughuli zake, na ilipofika jioni alijiandaa kurudi nyumbani na ndipo alipohisi utofauti kwenye macho yake, na mwisho kutoona kabisa kitendo kilichompeleka kuomba msaada wa kurudishwa nyumbani dereva bodaboda.
Doroth amesema kwamba ameshajaribu kupata tiba skwenye hospitali tofauti tofauti nchini humo na kujaribu kuwaona wataalam wa macho bil mafanikio yoyote, kitendo ambacho kinamuumiza sana kwani sasa anajiona mzigo kwa mume wake kwa kushindwa kufanya shughuli za kuingiza pesa kwa miezi 6 sasa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE