November 10, 2017

EXCLUSIVE :MSANII LULU AHUKUMIWA JELA MIAKA MIWILI...

Mahakama Kuu ya Tanzania, imemuhukumu miaka miwili jela muigizaji wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' baada ya kumtia hatiani katika kuuwa bila kukusudia.


Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema kuwa ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka.

Jaji Rumanyika amesema amemtia hatiani Lulu chini ya kifungu cha sheria namba 195 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Miongoni mwa sababu alizozitaja Jaji Rumanyika alisema kuwa 

Kesi ya upande wa mashtaka imejikita bara bara katika ushahidi wa mazingira na hakukuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja.

Alisema ni ushahidi wa mazingira na mshtakiwa alikubali kuwa yeye ni mtu wa mwisho kuwa na marehemu ambaye ni mpenzi wake waliodumu kwa miezi minne.

Alisema ushahidi wa mazingira unapaswa mshtakiwa kueleza kwa kina katika ushahidi wake pasipokuacha shaka.

Ushahidi wa mazingira unaweza kumtia hatiani mshtakiwa kama ushahidi utamnyooshea kidole moja kwa moja mshtakiwa.

"Nianze kwa kusema shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka alieleza alivyoeleza ambapo hata mshtakiwa alikiri alikuwa na marehemu,

Alisema katika ushahidi wa mshtakiwa alieleza kuwa alikuwa na mzozo na marehemu ambapo alianza kwa kumpiga, ambapo Mimi niliangalia tafsiri ya kugombana katika kamusi Kiingereza ya Coins ambapo tafsiri yake ni kama patashika.

Hivyo kuanguka kwa mmoja ama kusukumwa ni miongoni mwa mambo yanayotizamiwa katika kugombana.

Pia mshtakiwa alieleza katika ushahidi wake kuwa marehemu alikuwa amelewa na inatambulika kuwa miongoni mwa mambo ya walevi ni kuanguka mwenyewe.

Pia Jaji Rumanyika alisema mshtakiwa alijikanganya, akisema marehemu alimfukuza na kumkamata na kisha alifanikiwa kimburuza na kumuingiza chumbani.

Ila mshtakiwa hakuwahi kusema wakati mlevi huyu akimkimbiza aliwahi kuanguka ama kudondoka wakati akimkimbiza.

Kuhusu ushahidi wa Josephine Mushumbus kielelezo chake kinaacha maswali kwani maelezo yake sio ya cheti cha hospital kwani hayakuwa na adhi ya cheti cha Hospital.

Sababu ya pili katika kesi hii kongwe, Daktari Paplas Kagaila aliiambia mahakama hii na kujinadi kwamba yeye alikuwa ni Daktari wa familia, ila mahakama haikuambiwa kwamba Mushumbus naye alikuwa Daktari wa familia.

Hivyo ilitegemewa Daktari wa familia naye angetugaia historia ya marehemu, hivyo Daktari aliyepaswa kujua historian ya maradhi ya marehemu alipaswa kuwa dokta Paplas.

Pia mshtakiwa ambaye alikuwa mpenzi wa miezi minne wa marehemu alipaswa kujua historia ya mpenzi wake.

Pia ikizingatiwa hekma pale marehemu alipoanza kupigwa na marehemu, basi yeye hakufanya chochote hata kujitetea ni sawa na biblia kwamba ukipigwa shavu la kushoto mpe na lakulia.

Kwa msingi huo, tunabaki na watu wawili wa kuweza kulisemea ni mshtakiwa na marehemu, lakini hata ikitokea miujiza marehemu kafufuka na hata akifufuka mahakama haina miujiza ya kupokea ushahidi wake.

Hivyo kesi hii ina mazingira tofauti ambazo ni kuu tatu, mshtakiwa alikuwa ni mdogo, pia kuna wakati aliitwa mke na marehemu na akaitika.

Pia mtoto aina ya mshtakiwa ni yule asiyetii wazazi wake hata kufanya anayoyajua.

Pia mtoto aina ya mshtakiwa aliweza kutoka usiku na rafiki zake na kwenda kwa mpenzi wake na kuagana naye mambo ambayo Lulu ameyakiri.

Baada ya kuyasema hayo, huyu mshtakiwa sio wale watoto waliolengwa kulindwa na sheria ya watoto namba 13.

Nasema hivyo kwa maoni yangu, kwani kama mtoto anaweza kuyafanya mambo makubwa kiasi hicho, basi mahakama hii itegemee kuona hata wazee wanafanya mambo ya kitoto wakiamini watalindwa.

Kama mahakama zinaweza kuacha kufanya yale sheria ambayo hairuhusu basi jamii zetu zitakuwa hazina matazamio ya kisheria.

Hadi sasa najiridhisha kuwa kifo cha marehemu kimetokana na ugomvi ndio maana mshtakiwa yupo mahakamani, kwani vifo vya namna hiyo vinatokana na sababu hizo.

Nikijaribu kuangalia tafsiri ya kugombana ni ule mzozo unaoanzia kwa maneno na kusababisha kuvutana,

Hivyo sheria ya kuwa bila kukusudia inalengo la kutaka watu wasifanye hivyo na pia kuwapa tahadhari.

Hivyo kwa kuwa mshtakiwa amesema katika utetezi wake kwamba marehemu alikuwa na wivu uliovuka mipaka, itoshe kusema kama mapenzi ni Mchezo basi wivu ndio sehemu yake.

Kwa maneno mengine mshtakiwa alifahamu kwamba marehemu alikuwa na wivu, na kama alimfahamu kwa kiwango hicho hadi marehemu alipomshuku anaongea na simu alipaswa kumuacha.

Hivyo nalazimika kusema namtia hatiani mshtakiwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE