November 30, 2017

DACHENG ATEMBELEA SHULE YA SHERIA

IMG_20171130_114259
Naibu Waziri mhe. Zhao Dacheng akizungumza aliesimama kulia akizungumza wakati alipotembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam.
IMG_20171130_101109
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi  akizingumza wakati alipotembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam pamoja na mgeni wake Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng.
IMG_20171130_095039
Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam Prof. Hamudi Majamba akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Sheria wa China Mhe. Zhao  Dacheng alipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es  salaaam
IMG_20171130_122613
Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng wa tatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu Dar es salaam alipotembelea chuo hicho
…………….
Naibu Waziri wa Sheria wa China Mhe. Zhao Dacheng ametembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaaam.
Waziri Dacheng aliambatana na mwenyeji wake Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Katika ziara hiyo Waziri huyo wa China alipata fursa ya kujifunza jinsi Shule hiyo ya Sheria inavyotekeleza jukumu la kutoa msaada wa kisheria kwa umma wa watanzania wenye uhitaji.
Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam imekuwa ikitoa huduma ya msaada wa kisheria nchini kupitia walimu wao wenye vyeti vya uwakili, wanafunzi wake wa mwaka wa pili, wa tatu , wanne na wale ambao wanasubiria kujiunga na  Taasisi ya mafunzo kwa vitendo
Waziri huyo wa China yuko nchini kwa ziara ya siku nne ambapo anatembelea taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utoaji wa msaada wa sheria kwa watu wenye uhitaji nchini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE