November 21, 2017

BUNGE NCHINI ZIMBABWE LAANZA KUMJADILI MUGABE


Wabunge wametakiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kujadili hatma ya rais Mugabe
Chama tawala cha Zanu-Pf nchini Zimbabwe kimewataka wabunge wake kukutana na kujadili hatma ya rais Robert Mugabe, baada ya siku ya mwisho ya yeye kujiuzulu kupita.
Siku hiyo iliwekwa na chama cha Mugabe cha Zanu-Pf .
Mugabe anatarajiwa kujadiliwa bungeni kuanzia siku ya Jumanne ambapo anakabiliwa na shtaka la kumuachia mkewe kuwa na mamlaka ya kikatiba kulingana na chama tawala cha Zanu-Pf.
Kiongozi huyo anayepigwa vita aliwashangaza raia wengi wa Zimbabwe siku ya Jumapili alipotangaza katika runinga kwamba angependa kusalia kuwa rais.
Zanu-Pf kimesema kuwa kinaunga mkono hatua ya kuhoji uhalali wa rais Mugabe kuwa rais wa taifa hilo na kwamba mipango ya kumchukulia hatua hiyo inaweza kuanza siku ya Jumanne wakati bunge litakapokutana.
Katika muswada ulioonekana na kituo cha habari cha Reuters's chama hicho kimemlaumu rais huyo kwa kuharibu uchumi wa taifa hilo.
Uwezo wa rais Mugabe umepungua tangu jeshi kuingilia kati Jumatano iliopita kuhusu mzozo wa ni nani atakayemrithi.
Mgogoro huo ulianza wiki mbili zilizopita wakati kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa na hivyobasi kuwakasirisha makamanda wa jeshi ambao waliiona hatua hiyo kama ya kujaribu kumfanya mkewe kuwa mrithi wake.
Taifa hilo limeshuhudia maandamano makubwa ya kumtaka rais Mugabe kujiuzulu mara moja.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE